Kumbe Huwa Hawafanyi Haya.


Nkiongea na rafiki zangu, wengi huonekana wamekata tamaa na wanahisi hawajabahatika kufikia malengo yao.
Wengine wanahisi wamerogwa au kuna watu wanawachezea. Wanahisi wamekwama kiasi kwamba hawajui wafanye nini.
Mimi kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kuangalia vitu ambavyo hupoteza mda wao na kuwafanya wakwame. Vitu ambavyo huingia katika njia yao ya mafanikio.

Nafikri sote hufanya mambo ambayo hupoteza mda wetu. Nlikuwa nafanya hivyo kwa sana lakini nilibadilika baada ya kusoma kitabu kimoja kilichobadilisha mwelekeo wa maisha yangu.

Ni vizuri kuangalia ni kwa namna gani tunautumia mda saa kwa saa kwa kuondoa vikwazo ambavyo hututatiza njiani.
Tunaanza hapa kama ifuatavyo.

1. Watu waliofikia mafanikio huwa hawapitii siku bila mpango
Watu waliofanikiwa wana mpango, wanajua siku hiyo watafanya nini mpaka siku inaisha.

Rafiki yangu mmoja huwa ana imani sana katika kusoma vitabu na huwa haipiti siku bila yeye kusoma kitabu. Kila siku mpya yeye huipangia atasoma nini na kwa mda gani.
Utaratibu wake aliojiwekea ni kwamba kila siku anahakikisha anafanya mambo makubwa matatu, ambayo huyavunja katika malengo mengine madogo madogo na hivyo hujikuta akifurahia maisha kila siku na akitamani aweze kukamilisha kila kitu.

Jiwekee utaratibu wa kufanya mambo matatu kila siku na yavunje katika mambo madogo madogo kadiri ya vipaumbele vyako vilivyo. Anza kwa kufanya  vipaumbele vikubwa. Utajikuta unafurahia kila hatua unayopiga.

2. Watu waliofikia mafanikio hawafanyi mambo ya kuwarudisha nyuma. 
Watu waliofanikiwa hawajihusishi kabisa na mambo ambayo husababisha warudi nyuma kimaendeleo. Mfano; huwa hawajihusishi na kuvuta bangi au madawa ya kulevya ya aina yoyote.

Kwa hiyo kabla ya kufanya kitu, jiulize kile kitu kinaongeza thamani gani kwako?
Kama unafikiri hakiwezi, achana nacho. Na unapoulizwa swali, sio lazima utoe jibu la kitu fulani,  punde tu unapoulizwa. Jijengee utaratibu wa kufikiri kabla hujasema NDIO au HAPANA.

3. Watu wazalishaji na waliofikia mafanikio hawamezwi na mitandao.
Mitandao ya kijamii imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa watu kutembelea.  Kuangalia picha instagram, mambo mapya facebook, kutuma picha na video wasap. Yaani imekuwa ni sehemu ya kawaida ya maisha yetu.

Kiufupi kama hujajiwekea utaratibu ni mda gani utaingia mtandaoni na utafanya nini. Masaa yatapaa na  utashangaa masaa 24 yameisha na hujafanya chochote.
Jiwekee kikomo cha mda cha kuwa mtandaoni na lazima kiwe kidogo sana. Kama huwezi kujizuia weka hata alarm ili ikukumbushe ni mda gani sasa inabidi uzime data na kufanya mambo mengine kama ratiba yako ilivyo.

4. Watu waliofanikiwa huwa wanasoma vitabu.
Mara nyingi mtu akihitimu masomo basi anajiona kamaliza kila kitu. Kwa hiyo kumwambia asome vitabu kwake anaona ajabu.

Habari njema ni kwamba kusoma na kutafuta maarifa hakuna mwisho. Ni muhimu sana wewe kusoma na kujua mambo gani yanaendelea.
Mabadiliko gani yanatokea na jinsi ya kukabliana nayo.

Kusoma , kujifunza na kutafuta maarifa hakuna mwisho.

5. Watu waliofanikiwa hawana wasiwasi na mambo ambayo hawawezi kuyazuia.
Watu waliofanikiwa wanajua kuogopa hakuwezi kukupeleka kokote. Hasa pale unapokuwa huna uwezo wa kuzuia jambo.
Kwa hiyo badilisha mawazo yako, ili kushughulika na mambo ambayo utaweza kuzuia.

6. Watu waliofanikiwa  hawafanyi kile ambacho kila mtu anafanya.
Ni vizuri mtu kuvutiwa na mtu fulani kwa kile anachofanya. Lakini haupaswi kujifananisha na yeye. Watu waliofanikiwa huwa hawendelei na ratiba zilezile walizokuwa nazo zamani. Bali hubadili ratiba zao na kufanya jambo kwa kuliongezea thamani.

Ukifanya kile kitu ambacho kila mtu anafanya haiwezi kukupa utaofauti na hivyo itawapelekea watu kuona ni mambo yaleyale tu waliyozoea kutoka kwa watu wengine. Ebu jitofautishe na watu wengine kwa kufanya kile ambacho hawafanyi.

7. Watu waliofanikiwa hawawazii makosa ya zamani.
Watu waliofanikiwa hufanya makosa sana. Moja ya mbinu ambazo huzitumia watu waliofanikiwa ni kutorudia kosa lilelile kila siku. Huwa wanafanya mabadiliko makubwa kutokana na makosa yao na hivyo kupiga hatua kimaendeleo.

Endelea kusoma makala kutoka SONGA MBELE BLOG kila siku.

Ni mimi ndugu yako,
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X