Je, wewe Una Matamanio Au Ndoto?


Kwa kawaida kila mtu huwa ana kuna vitu vuzuri ambavyo angependa kuvifikia maishani mwake. Ni mafanikio ambayo hupenda kuyafikia. Mambo yote ambayo binadamu hufikria huweza kuwekwa katika makundi mawili.

Kundi la kwanza ni matamanio
Hili ni kundi ambalo mtu huwa anataka kuwa mtu fulani au kufikia mafanikio fulani bila kuweka juhudi. Ebu tuchukulie mtu anataka kuwa mchezaji maarufu sana duniani katika mpira wa miguu, lakini hajweka juhudi za kufanya mazoezi na ratiba yake ya kila siku ni kuamka saa mbili, baada ya hapo anapata chai, matembezi,mlo wa mchana, jioni kuzurura na usiku kuangalia movie. Hivi kweli mtu huyu anaweza kuwa mchezaji maarufu duniani. Kwa haraka hapa kutokana na ratiba yake hawezi kuwa mchezaji maarufu.
Au mwingine anataka kuwa msanii maarufu sana, halafu haweki juhudi kuhakikisha anafikia mafanikio ya ndoto yake. Hajweka juhudi zozote kuhakikisha anafikia anapotaka kufikia.
Siku zote iki uweze kufikia malengo na ndoto zako nzuri lazima uwe na ratiba ya tofauti. Kama unafanya kile kila mtu anafanya basi huwezi kufika mbali kimafanikio.  Siku zote watu waliofikia mafanikio wanafanya mambo ya tofauti na ni wabunifu.

Soma zaidi hapa; Jinsi ya Kuepuka Kauli Hizi Tatu (03) za Kukatisha Tamaa

# Kundi la pili ni la watu wenye ndoto.
Watu wenye ndoto ni wale ambao maisha yao ya baadae wanayaona jinsi yatakavyokuwa na wanawekeza malengo na mipango ili kuweza kuyafikia.
Katika mifano yetu ya hapo juu ebu chukulia mtu mwingine anataka kuwa mchezaji bora duniani, na ana nafasi mbili za mazoezi ya kila siku asubuhi na jioni. Na mda wote yeye anafikiri juu ya ya ndoto yake ya kuwa mchezaji bora duniani. Je ataweza kuwa mchezaji bora duniani?
Au mwingine anapenda  kuwa mwanamziki bora duniani na ratiba yake ni kama ifuatavyo. Anaamka asubuhi na mapema na kuanza kutunga miziki na kuimba, lakini pia mchana ana ratiba ya kuonana na watu ambao tayari wanafanya vizuri kwenye mziki. Jioni ana ratiba nyingine tena ya kuimba na kufanya mazoezi ya ala za mziki. Je, huyu ataweza kuwa mwanamziki maarufu duniani?

Soma zaidi hapa; Ufahamu Uovu wa Lazima Kwenye Maisha Yako

Kumbe siku zote inabidi kila mtu awe wa kupanga mipango na kuweka ndoto za kumfikisha kwenye mafanikio. Ebu anza sasa kuifanyia kazi ndoto yako ili uweze kuifikia. Usiifiche ndoto na kusubiri mpaka utakapokuwa maarufu. Kwa uhakika hutaweza kuwa maarufu kama hujaanza sasa,hujabadilika sasa na hujatambua kwamba mda ni sasa na hakuna mda mwingine kama sasa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii.

Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maarumu za kila wiki bonyeza hapa

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X