Hili ni Jambo la Pekee Ambalo Huwezi Kuliepuka


Habari za leo ndugu msomaji wa SONGAMBELE BLOG. 
Ni imani yangu unaendelea vyema katika safari ya kuelekea mafanikio. Leo hii tunaenda kujifunza jambo la muhimu na pekee sana ambalo huwezi kuliepuka. Jambo hili utapaswa kulifanya kila siku ili maisha yako yaweze kufikia mafanikio.
Je jambo lenyewe ni lipi?

Soma; Ukweli Kuhusu Safari ya Mafanikio

Jambo lenyewe ni mabadiliko. Mabadiliko ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa sana siku hizi na watu mbalimbali. Watu wamekuwa wakiitaka serikali ifanye mabadiliko  katika mifumo yake ya kitutendaji mahakama zibadilike na zitende haki na mambo mengine mengi.

Soma; jinsi ya kuepuka kujiua mwenyewe kiakili

Dhana nzima ya mabadiliko kiukweli haianzi na serikali, taasisi au jumuiya.
Dhana nzima ya mabadiliko inaanza na wewe mwenyewe. Mabadiliko hayawezi kutokea kama wewe hujabadilika kwanza.

Mabadiliko ni mipango, mabadiliko si ya kuzungumza kwa jumlajumla na hayaji kama mvua kama ambavyo watu wengi hufikiria. Mabadiliko ni hatua.
Mabadiliko si kama mafuriko kwamba yakipita kila kitu kimeharibika. Mabadiliko ni mchakato na unaweza kuchukua mda mrefu kufikia mabadiliko yaliyodhaniwa.

Sio kwamba nakatisha tamaa, juu ya suala zima la mabdiliko bali nataka tuone uhalisia ulio katika mabadiliko na tuufuate. Kuna mambo mengi sana ambayo hubadilika kila siku na kubadilika kwake huleta faida kwetu. Mfano wa mabadiliko ambayo hutokea ni mabadiliko katika mfumo wetu wa chakula hutuletea faida kubwa sana. Ukila mhogo, unamengenywa na kukatwakatwa na kutoa glukozi ambayo ndio huvunjwa vunjwa mpaka pale unapopata nguvu. Sio muhogo ambao umeleta nguvu bali baada ya mabadiko kilichitokea ndicho kimeleta nguvu.
Haya ndiyo mabadiliko ambayo yametokea katika suala zima la kupata nguvu.

Soma; Kama Hawa Wameweza Kwa Nini Wewe Usiweze

Vivyo hivyo katika maendeleo ni lazima maendeleo yatokee lakini lazima yataanza na wewe.
Badilisha kwanza mtazamo wako, badilisha familia ndugu jamaa na marafiki. Huwezi kukimbia kuwaambia wengine badilika wakati wewe hujabadilika.

Nakutakia safari njema ya kuelekea mafanikio na mabadiliko ili uweze kufanikiwa na kufikia matokeo makubwa.

Endelea kusoma makaka za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


4 responses to “Hili ni Jambo la Pekee Ambalo Huwezi Kuliepuka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X