Sheria Muhimu Katika Kutengeneza Pesa Na Kuwa Tajiri


Watu wengi wamekuwa na ndoto kubwa sana ya kuwa matajiri.Lakini hawajapata kujua jambo muhimu katika kutengeneza pesa na hivyo kufikia ndoto yao ya kuwa tajiri.

Jambo muhimu unalohitaji kulifahamu katika kutengeneza pesa ni kufahamu tofauti kati ya RASLIMALI (asset) na DHIMA (liability).

Swali Rasilimali ni nini? Rasilimali ni kitu kinachoingiza pesa kwenye mfuko wako Swali dhima ni nini?Dhima ni kitu kinachotoa pesa kwenye mfuko wako.

Ni kitu ambacho ukishakinunua kitaendelea kukugharimu pesa kukiendesha. Wakati raslimali zinaingiza pesa kwenye mfuko sehem ya kipato na hivyo kukufanya ukue kiuchumi. Dhima hutoa pesa kwenye mfuko wako na hivyo kupunguza pesa zilizo kwenye kipato.

Kadri mtu unavyokuwa na raslimali nyingi ndivyo na kipato chako kinavyokua na hivyo kukuweka katika hali nzuri kiuchumi. Anza leo kununua raslimali ili uweze kuongeza kipato chako.

Ni mimi rafiki na ndugu yako Godius Rweyongeza Endelea kufuatilia makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka katika blogu hii

Soma zaidi: Sababu 5 Kwa Nini Haupaswi Kuomba Fedha Kwa Wazazi: Jifunze Kujitegemea na Kuwekeza Kwa Mafanikio

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie godiusrweyongeza1@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

For Consultation only: +255 755 848 391

,

One response to “Sheria Muhimu Katika Kutengeneza Pesa Na Kuwa Tajiri”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X