Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati wa Kuanzisha Biashara


Wakati wa hali mbaya kiuchumi na mshahara kidogo  kwa walioajiriwa vikipamba moto ,wazo la kuanzisha biashara na kuwa bosi wako mwenyewe linaweza kuwa bora zaidi.
Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara

1.Wazo
Katika kila wazo zuri la biashara ulilo nalo kuna mamia ya watu wana wazo hilohilo.

  • Jambo muhimu la kuzingatia ni kama wazo lako lipo,au je kuna watu tayari  wanafanyia kazi wazo lako? Kama jibu ni ndio jiulize je,unaweza kupata wazo jingine au kufanya biashara hiyohiyo kwa kujitofautisha na watangulizi wako?
  • Jiulize maswali yafuatayo: Je,kuna mpango mzuri wa biashara? Je watu wengine wanaofanya biashara hiyohiyo wanatengeneza hela? Kama wanapata nini nifanye ili nifanikiwe na niingize hela zaidi yao?
  • Mwisho unahitaji kujua kama wazo lako kisheria linakubalika au la!
2.Mpango wa biashara
Tengeneza mpango wa biahara . Watu wengi huwa wanaruka kipengele hiki na kuanza moja kwa moja biashara na hatimae biashara zao huishia njiani. Kutengeneza mpango wako utakusaidia kulinda mtazamo wako na mwelekeo wako kibiashara. Fikiria mpango wa biashara yako kama kitu muhimu sana. Huwezi kuanza kujenga nyumba bila ramani.
3.Upekee wa biashara 
Amua biashara yako isimame kwa namna gani,lazima uwe na ushindani kwenye biashara yako utakao kutofautisha wewe na washindani wako.Ipe thamani biashara yako.
4.Nani yuko kwenye gari lako 
Tambua kwamba wewe ndo dereva na gari ni kampuni au biashara yako na bado limesimama au halijaanza safari.Amua unaenda wapi? Amua unaenda na akina nani? Amua unataka kufika wapi?
Utaendesha biashara peke yako au unahaji watu wa kuajiri?
5.Umuhimu wa mteja.
Soko lako kuu ni lipi? Kabla ya kupanga mbinu za kuuza unahitaji kujua soko lako lengwa ni lipi? Soko lengwa ni kikundi cha watu ambacho kampuni yako imetengeza bidhaa kwa ajili yake.
6.www.kampuniyako .com
Tengeneza tovuti au blogu maarumu kwa ajili ya biashara yako. Haijalishi utakuwa unatengeneza matofali au utakuwa ukilima kuwa na  tovuti au blogu ni muhimu sana. Blogu yako itakuweka mbele kuweza kuuza biashara yako mtandaoni. Ni muhimu pia wewe  kuwa na email kwa ajili ya biashara yako.
7.Mwonekank wako wa kwanza (first impression)
Una mbinu gani ya kwenda sokoni? Utawezaje kuwashawishi watu? Elewa mambo gani ni muhimu ili kuliteka soko? Kuelewa mbinu gani ni muhimu sana hasa pale watu wanapokuwa hawajui kama bidhaa yako ipo? Wapi inapatikana? Na namna ya kuinunua?
8.Fahamu jinsi ya kuipiga tafu biashara.
Je hela ya kuanzisha na kuendesha biashara itatoka wapi?Hili linaweza kuwa jambo ambalo linasumbua ila fuatilia kujua wengine waliwezaje kufanya biashara zao. Je, utalipwaje? Kama ni tigo pesa mpesa au keshi ya mkononi.
9. Je una elimu ya kutosha?
Kitu cha kwanza tunasikia kutoka kwa wafanya biashara wanasema ningelijua.hii inaonesha wazi huyu mtu hakufuatilia kwa umakini biashara yake kabla ya kuianza. Jiandae kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza na kuifanyia kazi.
10.Uko wapi mlango wa kutokea?
Mlango wa kuyokea ni muhimu sana.Kama biashara yako itakua (na lazima itakua).
Utataka kuiuza ili kutengeneza faida kubwa?Kama utakuja kuiuza biahara yako unapaswa kuanza biashara yako tangu siku ya kwanza ukijua ipo siku utakuja kuiuza. Kwa hiyo anza kuweka rekodi nzuri za mapato,matumizi,manunuzi pamoja na mauzo.
11.Soma. Soma. Soma.  
Ni muhimu sana kufuatilia biashara yako kwa kusoma makala na vitabu mbalimbali vinavyohusu biashara hiyo.Hii itakujengea msingi mzuri katika biashara lakini pia utaweza kujua mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye biashara usiku na mchana.
Hivyo nasisitiza tena endelea kusoma kila siku ili ujue ni mabadiliko gani yanatokea kwenye biashara yako. Endelea pia kufuatilia www.songambeleadress.blogspot.com kila siku.
Ni mimi ndugu yako 
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane.
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante sana 
songambeleadress.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X