Jinsi Ya Kuepuka Kujiua Mwengewe Kiakili


Kujiua mwenyewe kiakili ni pale ubongo unapojirarua mwenyewe.Mwili unataka kufanya jambo fulani lakini ubongo ushakata tamaa na unaamua kujiua.

Kila kitu tunachofikiria kinaweza kukujenga au kukubomoa.Kina uwezo wa kukutoa sehemu ya chini kimaendeleo na kukupeleka sehemu ya juu.Uko ulivyo kwa sababu ya jinsi unavyofikria,ukijisemea
mimi  ni maskini
Au hiki sikiwezi
Au mimi ni mvivu utabaki kuwa hivyo hivyo tu siku zote.
Kwa nini? Kwa sababu kile unachojaza kwenye sehemu ya akili inayoitwa SUB CONSIOUS MIND ndicho unachokuwa.
ukijisemea mimi ni mshindi utashinda tu.
Na ukijisemea mimi ni mshindwa utashindwa tu.
Subconsious mind huwa haina uwezo wa uzalisha mawazo bali huwa inafanyia kazi kile ambacho wewe unafikiria.Na kile unachofikiria kinaanzia kwenye kile kinaitwa na wana saikolojia AUTO SUGESTION.   Humu ndipo hutoka mawazo yote mazuri na mabaya,hivyo yakupasa kuwa mtu wa kufikiri mawazo ya kujenga tu.
Kama vile upepo unavyoweza kukutoa mashariki na kukupeleka magharibi vivyo hivyo kinachotoka kwenye auto sugestion kinaweza kukuinua juu au kukushusha chini.
Ebu tusome shairi hili kwa umakini
Kama unafikiria umepigwa,umepigwa
Kama unafikiri umeshindwa,umeshindwa
Kama unafikiri huwezi,huwezi
Kama unataka kushinda lakini unafikiri huwezi,karbia huwezi.

Kama unafikiri utapoteza,umepotea
Kwa sababu katika dunia ushindi unaanza na msukumo wa ndani ya mtu,
Hiyo inaitwa hali ya akili.(state of mind).
Kama unafikiri umepitwa na wakati,umepitwa
Inabidi ufikiri mbali kujiinua
Inabdi ujiamini mwenyewe kabla ya kushinda tuzo.
Vita vya maisha hashindi mtu mweye nguvu au mwenye mbio za haraka
Vita vya maisha anashinda mtu ANAYEFIKIRI ANAWEZA.


Ukiangalia maneno yaliyowekewa mkazo utagundua mshairi alikuwa anataka kusisitiza nini.
Kwa hiyo mbegu kubwa ya mafanikio imo kwenye mwili wako( labda kwenye seli za ubongo wako) imelala  ukiiamsha itakubeba kiasi ambacho wewe usingetegemea.
Kwa hiyo wakati wa kuamsha mbegu hiyo ni sasa.
Anza sasa kufikiri katika hali chanya
Nakutakia mafanikio mema
Ni mimi ndugu yako 
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane 
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Endelea kusoma makala zaidi katika blogu hii za kuelimisha na kuhamasisha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X