Faida 6 za Kusoma Vitabu na Makala za Kuelimisha.


Habari za leo msomaji wa songambeleadress.blogspot.com ni imani yangu kuwa unaendelea vyema katika hatua za kuweza kufikia malengo uliyojiwekea

Leo ningependa tujue umuhimu wa kusona vitabu na makala za kuelimisha, lakini pia tujifunze na kuanza kujisomea vitabu.

1.Unapata kujua mambo mapya.
Kupitia kusoma unapata kujua vitu vipya,taarifa mpya na mbinu mpya za kutatua matatizo Ili uweze kupata yote haya lazima uanze kusoma.
Anza leo jiwekee utaratibu wa kusoma vitabu kila siku lakini pia jiwekee utaratibu wa kusoma makala za kuelimisha kila siku.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi Wa Kitabu Cha The 5Am Club: (Mambo 304 niliyojifunza kutoka kwenye hiki kitabu)

2.Ukuaji binafsi.
Kusoma kunakufanya wewe ukue kiakili, unaanza kuielewa dunia taratibu na unaanza kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya muhimu
Kwa mfano;Unajua umuhimu wa kujiamini,namna ya kutengeneza mipango kabla ya kuchukua hatua,namna ya kukariri mambo vizuri na haraka vitu hivi vyote huanzia kwenye kusoma vitabu. Kupitia kusoma unaelewa  njia ya kuendelea mbele na mbinu za kuchukua ili kufikia mafanikio.

SOMA ZAIDI: KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI: MWONGOZO WENYE HATUA ZA KUFUATA MWANZO MPAKA MWISHO (Usome kwa manufaa yako, upuuze kwa hasara yako

3.Unaongeza uelewa.
Kadri unavyosoma ndivyo unavyoelewa kitu kimoja baada ya kingine,na unakielewa mwanzo hadi mwisho. Kusoma pia kunakufanya uweze kuishi katika jamii vizuri. Unaweza kujua namna ya kuanzisha biashara,namna ya kuhudumia wateja wako,namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika biashara n.k.

SOMA ZAIDI: Kitabu: How to Win Friends and Influence People

4.Maandalizi kabla ya jambo lolote.
Kabla hujachukua hatua yoyote unaweza kupata wapi msaada na mwongozo? Ni kupitia kusoma. Katika dunia ya sasa kujua faida na hasara ni muhimu, kujua taarifa za watu waliofanya jambo fulani na wakashindwa kufanikiwa kutakusaidia kujua wakikosea wapi na hivyo kujipanga kutatua changamoto walizo kutana nazo wengine.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi wa Kitabu: The Leader Who Had no Title (Kiongozi Asiye na Cheo); Mambo 200 Niliyojifunza katika kitabu hiki.

5.Unapata ujuzi kutoka kwa watu wengine.
Unapokuwa mtu wa kusoma unapata ujuzi kutoka kwa watu wengine.Hii inaweza kukusaidia kuleta maendekeo ya haraka kwenye malengo yako.
Katika dunia ya sasa kuna mabilionea zaidi ya 4000 na mamilionea zaidi ya elfu 12 .
Ili kufikia mafanikio aliyoyafikia mmoja wapo unahitaji kusoma na kujua, ni kwa namna gani ameweza  kufikia mafanikio? Ni mbinu gani ametumia kuweza kufikia mafanikio? Changamoto gani amepitia? Amezitatuaje? Hayo yote hukurahisishia mwelekeo wa kufikia mafanikio kwani huhitaji kurudia makosa yaleyale yaliyofanywa na mtangulizi wako.

SOMA ZAIDI: Jinsi Ya Kushughulika Na Fedha Unazopata Kutokana Na Kipaji Chako 

6.Ni njia ya kuwasiliana .
Tupo kwenye zama za taarifa ambapo mtu mwenye taarifa sahihi na anyeifikisha kwa hadhira ndani ya mda sahihi ndiye anatengeneza pesa. Huwezi kupata taarifa sahihi kama wewe sio mtu wa kusoma na kujua mabadikiko yanayotokea katika dunia hii.
Huwezi kuwashirikisha wenzako jambo jipya kana wewe sio mtu wa kusoma.
 Kumbe ni muhimu sana wewe kuanza kusoma sasa ili kujipatia taarifa sahihi kwa mda sahihi
Unahitaji kusoma nakujua mambo yanayoendelea na kujua jinsi ya kukabiliana na mbadikiko.

SOMA ZAIDI: maeneo matano Unayopaswa kuyawekea NGUVU mwaka 2024 kwenye kusoma na kujifunza na vitabu Unayopaswa kusoma.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

 

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

Endelea kutembelea songambeleadress blogspot.com kila siku.
Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza 
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X